Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ulianzishwa rasmi mwaka 1978, ukiwa ni muunganiko wa Afro-Shirazi Party Youth League (ASP-YL) ya Zanzibar na TANU Youth League (TYL) ya Tanganyika. Tangu kuanzishwa kwake, umekuwa chombo kikuu cha Chama katika kuandaa na kuwalea vijana kuwa viongozi na raia wema.
Kwa zaidi ya miaka 40 sasa, UVCCM imekuwa kiungo muhimu katika kuhakikisha kwamba sauti ya vijana inasikika katika mchakato wa kisiasa na maendeleo ya nchi. Umoja huu umejitolea kwa muda mrefu katika kukuza ujasiriamali wa vijana, uwezeshaji wa kiuchumi, na ustawi wa kijamii.
UVCCM ilianzishwa mwaka 1978 baada ya muungano wa ASP-YL na TYL
Idadi ya wanachama waliosajiliwa kwa sasa
Tunaamini kwamba binadamu wote ni sawa, na kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Imani yetu inajikita katika kuondoa aina zote za ubaguzi, unyonyaji, na rushwa, na kujenga jamii yenye usawa, haki, na amani.
UVCCM inaamini katika nguvu ya vijana kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Tunasisitiza umuhimu wa:
Kujenga mazingira ya ushirikiano kati ya vijana
Kuhimiza ubunifu na ujasiriamali wa vijana
Itikadi ya UVCCM ni Ujamaa na Kujitegemea. Inasisitiza umuhimu wa kujenga uchumi imara unaomilikiwa na wananchi, huku serikali ikiweka mazingira wezeshi. Tunahimiza uzalishaji mali kwa pamoja na mgawanyo sawa wa matunda ya jasho la wwwww
UVCCM ina malengo makubwa ya kuhakikisha kwamba vijana wa Tanzania wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi na kuwa viongozi wa kesho. Malengo yetu makuu in pamoja na:
Itikadi ya UVCCM ni Ujamaa na Kujitegemea. Inasisitiza umuhimu wa kujenga uchumi imara unaomilikiwa na wananchi, huku serikali ikiweka mazingira wezeshi. Tunahimiza uzalishaji mali kwa pamoja na mgawanyo sawa wa matunda ya jasho