TRILIONI 2.4 ZA RAIS DKT. SAMIA ZAAMSHA MUITIKIO MKUBWA KWA VIJANA WASOMI DAR ES SALAAM
Dar es Salaam, 23 Desemba 2025 Maelfu ya vijana wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika Hafla ya Ukaribisho wa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, chini ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC).
Soma Zaidi
ATAKAYECHEZEA AMANI YA TAIFA LETU AWE ADUI YETU SOTE
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ametoa wito kwa vijana wote wa Kitanzania, viongozi na wananchi kwa ujumla kulinda, kutetea na kudumisha amani ya Taifa letu. Amesisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu muhimu na ya msingi kwa ustawi wa Taifa, akibainisha kuwa yeyote atakayethubutu kuichezea amani hiyo hana nafasi katika jamii na anapaswa kuonekana kuwa adui wa wote.
Soma Zaidi
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Rais wa Tanzania
Dar es Salaam | 14 Disemba 2025 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Antonio Guterres, ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa kielelezo cha amani, mshikamano wa kijamii na utulivu wa kisiasa barani Afrika na duniani, licha ya changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Soma Zaidi
TAARIFA KUTOKA KWA MHESHIMIWA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Uhuru Kesho, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri Mkuu leo, ametoa agizo maalum kwa wananchi wote wa Tanzania.
Soma Zaidi
Tanzania na Marekani Zimefikisha Hatua za Mwisho za Kufanikisha Makubaliano Makubwa ya Uwekezaji
Dodoma, Tanzania – Tanzania na Marekani ziko katika hatua za mwisho za kufanikisha makubaliano makubwa ya uwekezaji yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kiusalama kati ya mataifa haya mawili. Hii ni hatua inayothibitisha dhamira ya pande zote mbili katika kujenga ushirikiano wa kisasa, unaolenga ustawi wa pamoja.
Soma Zaidi
Jessica Mshama atoa pongezi kwa Viongozi wa Vijana Walioshiriki Katika Kikao Kazi cha UVCCM Mkoa wa Dodoma
DODOMA, TANZANIA — Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imetoa shukrani na pongezi za kipekee kwa viongozi wote wa vijana waliohudhuria kikao kazi cha Umoja wa Vijana kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 7 Desemba 2025 ambapo washiriki walijadiliana juu ya mustakabali wa vijana, amani ya nchi na maendeleo ya taifa.
Soma Zaidi