HONGERENI SANA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2025
14 Oct, 2025
52 Machapisho
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida(MCC) unatoa hongera na pongezi kwa Vijana wenzetu Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 kwa kazi kubwa ya kizalendo, ushujaa, uadilifu na kujitoa kwa moyo mmoja kulitumikia taifa letu.
Tunawapongeza Ndugu Ahmada Hamisi Ahmada, Ndugu Zainabu Suleiman Mbwana, Ndugu Azizi Juma Aboubakar, Ndugu Elizabeth Petro Makingi na Ndugu Comrade Ismail Ali Ussi ambaye ndiye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025. Hongereni sana kwa kuhitimisha kwa mafanikio makubwa mbio za mwaka huu zilizofanyika Mkoani Mbeya, tarehe 14 Oktoba 2025, baada ya safari ndefu na yenye mafanikio mliyoianza Kibaha, Mkoa wa Pwani, tarehe 02 Aprili 2025.
Kwa siku 195 sawa na miezi sita na nusu mmezunguka mikoa yote 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkihamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, mkisisitiza amani, umoja, upendo na mshikamano kama msingi wa taifa lenye ustawi. Mmekuwa vijana bora wa mfano kwetu, uongozi bora, nidhamu na moyo wa kizalendo kwa taifa letu.
Tukikumbuka historia, Mwenge wa Uhuru ni alama ya matumaini iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa nia ya: “Kuletea matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale penye chuki na heshima pale palipojaa dharau.â€
Kwa namna ya kipekee, UVCCM tunampongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Comrade Ismail Ali Ussi, kwa uongozi wake makini, nidhamu na uthubutu uliowezesha timu kufanikisha mbio hizi kwa mafanikio makubwa na kuendeleza heshima ya taifa letu na heshima ya sisi vijana.
Hongereni sana wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 mmeandika historia ya ushujaa, uzalendo na umoja wa Watanzania.
Kauli mbiu:“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.â€
#KazinaUtuTunasongaMbele
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo