UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI CCM KULETA BOTI MBILI ZA KUSAFIRISHA WAGONJWA MULEBA

15 Oct, 2025 5 Machapisho
🗓️ Tarehe 15 Oktoba 2025
📍Muleba-Kagera

Katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wanaoishi katika visiwa na Maeneo ya Mwambao wa Ziwa Victoria, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango wa serikali wa kuleta boti mbili mpya za kisasa kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa katika Halmashauri ya Muleba, Mkoa wa Kagera. 

Dkt. Samia amesema hatua hiyo Inalenga kupunguza Vifo vya mama Wajawazito na wagonjwa wanaoshindwa kufika Hospitalini kwa wakati, Sambamba na Kuendeleza jitihada za Awamu ya Sita za kuimarisha huduma za afya hadi katika maeneo ya mbali, Uamuzi huu unaonyesha dhamira ya kweli ya serikali ya CCM kuhakikisha hakuna Mtanzania anayepoteza maisha kwa sababu ya umbali au Ukosefu wa usafiri wa dharura hivyo kuendeleza falsafa ya maendeleo yenye kugusa maisha ya watu Moja kwa Moja.

#oktobatunatiki✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅