UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

AHSANTE KAGERA KWA MAPOKEZI MAZURI YA ILANI YA CCM

17 Oct, 2025 11 Machapisho
📍Kagera - Tanzania
🗓️ Alhamisi16 Oktoba, 2025

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi Chini ya Mwenyekiti wake Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya mkoa wa Kagera leo na kuahidi ahadi zifuatazo zilizopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya mkoa wa Kagera;

AFYA
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejipanga kuboresha Huduma ya Afya kwa Nchi nzima kwa kutoa Bima ya Afya kwa watu wote ndani ya nchi itakayopelekea kupunguza vifo ndani ya Nchi. 
Pia kwenye Sekta ya Afya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejipanga kwa siku 100 zijazo za kwanza baada ya Uchaguzi, kuwaajiri wataalam mbalimbali kwenye Sekta hii kwa lengo la kuboresha Sekta ya Afya.

ELIMU
Mgombea wa kiti Cha urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi yuko Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi Uboreshaji wa Sekta Ya Elimu kwa kufanya ujenzi wa Mabweni kwa Shule za Sekondari, Na kutunisha mifuko Ya Elimu ya juu ili vijana wanaomaliza kidato cha Sita. 

UMEME
Serikali ya CCM inaenda kumaliza Changamoto ya umeme kwa kujenga kituo cha kupokea na kupooza umeme ndani ya mkoa Wa Kagera ili kuwa na Umeme wa uhakika ndani ya masaa 24 kwa Mwaka.

#oktobatunatiki
#fyuchabilastresi
#tokanitoketukatiki