UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

TANZANIA INASHIKA NAFASI YA PILI UZALISHAJI MAHINDI NA TUMBAKU AFRIKA

20 Oct, 2025 9 Machapisho
Mkuranga - Pwani, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mgombea wa kiti Cha urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Leo akiwa Mkoani Pwani akiendelea kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi ameeleza kuwa Tanzania tumefikia hatua nzuri ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na Tumbaku inayosaidia katika kukuza Uchumi wa Nchi.

Pia Dkt Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Mazao ya Mahindi yanasaidia kwenye swala la uzalishaji wa Chakula kinachotumika  Ndani ya Nchi na kwa asilimia kubwa imetokomeza tatizo la Njaa ndani ya Taifa letu la Tanzania. 

#oktobatunatiki ✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅