RAIS DKT. SAMIA: WATANZANIA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LIDUMU KATIKA AMANI
16 Nov, 2025
85 Machapisho
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumapili, Novemba 16, 2025) alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu.â€
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii.
“Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani hatuwezi kuendesha ibada. Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu. Pakiwa na amani tunaweza kutekeleza yale yaliyo katika matarajio yetu, tunaweza hata kutatua yale tunayoyaona kuwa ni magumu.â€
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Christian Ndossa ambaye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waishi kwa kumtanguliza Mungu mbele na wawe na matumaini kwake na wajiepushe na maovu.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mwenza wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, katika ibada hiyo.
Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo, Mbunge wa Kilolo, Ritha Kabati, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, Mbunge wa Viti Maalumu, Balozi Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Itigi, Yohana Msita na Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga.
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko