KAWAIDA: VIJANA, TUNAJUKUMU LA KULINDA AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAIFA LETU
07 Dec, 2025
73 Machapisho
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mohammed Ali Kawaida(MCC) amesisitiza wito wa mshikamano na amani miongoni mwa Watanzania, huku akibainisha mafanikio makubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dodoma, 07 Desemba 2025 – Katika Kikao Kazi cha Viongozi wa UVCCM ngazi ya Taifa, Mikoa, Wilaya na Seneti kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Kawaida amewaomba vijana na Watanzania wote kutotumika kuharibu amani ya nchi.
"Niwaombe tena na tena, Vijana na Watanzania wote, tusiendelee kujiumiza wenyewe kwa kushawishiwa na watu ambao hawapo Tanzania. Hatuna nchi nyingine. Nchi yetu ni Tanzania; lazima tuilinde na tuiheshimu," alisema Kawaida.
Kawaida pia amesisitiza mafanikio ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan:
- Kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi
- Ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya, na zahanati
- Kuendeleza elimu kupitia shule na vyuo vya VETA
- Kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari
- Kufutwa kwa kesi za kisiasa
Maoni ya Mwandishi: Kwa mtazamo wangu, hotuba ya Kawaida inasisitiza mshikamano na amani lakink pia inawakumbusha vijana kuwa maendeleo ya taifa hayaji kwa bahati, bali kwa ushirikiano, uwajibikaji, na upendo kwa nchi. Kwa hakika, wito huu ni sahihi katika mazingira ya kisiasa ambapo amani na mshikamano vinaweza kudhuriwa na watu wenye nia mbaya. Hii ni fursa kwa vijana kuonyesha uzalendo wao kwa vitendo, sio maneno tu.
Kikao hiki kinaonesha wazi dhamira UVCCM katika kukuza uzalendo, mshikamano wa kitaifa, na ushirikiano miongoni mwa vijana wote wa Kitanzania.Kawaida amehimiza kuwa kila Mtanzania ana jukumu la kulinda amani na mshikamano wa taifa, jambo linalopaswa kuwa kielelezo cha kila kijana anayependa Tanzania.
#KazinaUtutunasongambele
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo