Jessica Mshama atoa pongezi kwa Viongozi wa Vijana Walioshiriki Katika Kikao Kazi cha UVCCM Mkoa wa Dodoma
07 Dec, 2025
46 Machapisho
DODOMA, TANZANIA — Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imetoa shukrani na pongezi za kipekee kwa viongozi wote wa vijana waliohudhuria kikao kazi cha Umoja wa Vijana kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 7 Desemba 2025 ambapo washiriki walijadiliana juu ya mustakabali wa vijana, amani ya nchi na maendeleo ya taifa.
Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya idara, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM, Ndugu Jessica Mshama, alisema kuwa mwitikio mkubwa wa viongozi wa vijana kutoka ngazi ya Taifa, Makatibu wa Vijana, Makatibu wa Hamasa, pamoja na viongozi wa Seneti, umeonyesha kwa mara nyingine dhamira njema ya kulinda na kuendeleza misingi ya umoja, uzalendo, amani na maendeleo nchini.
“Ushiriki wenu umetudhihirishia kwamba tunabeba dhamana ya vijana wa Taifa kwa umoja, uzalendo na kwa dhamiri ya kutumikia nchi yetu. Mmekuwa mfano wa uongozi makini unaoenzi misingi ya maadili, mshikamano na uwajibikaji,†alisema Jessica Mshama.
Aidha, alisisitiza kuwa UVCCM inaendelea kuthamini mawazo, mchango na mjadala mzito uliotolewa na vijana katika kikao hicho, akisema kuwa nguvu, nidhamu na ari ya viongozi hao imeendelea kuipa nguvu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi kusukuma mbele ajenda za maendeleo na ustawi wa vijana.
“Nawakumbusha kuendelea kusimama imara, kutekeleza kwa ukamilifu maelekezo yote tuliyopokea, na kuendeleza hamasa za amani na maendeleo popote tulipo. Sisi ni viongozi wa fikra, viongozi wa maendeleo, na viongozi wa amani,†aliongeza.
Katika salamu zake, Jessica aliwapongeza pia viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa usimamizi bora wa jumuiya, akitoa shukrani za pekee kwa Mgeni Rasmi wa kikao, Ndugu Kenani Kihongosi, kwa uwepo na mchango wake katika majadiliano.
Vilevile, alitoa pongezi maalumu kwa Mwenyekiti wa UVCCM Tanzania Ndugu Comrade Kawaida(MCC) kwa uongozi wake imara na mwanga kwa vijana wanaoendeleza kazi za CCM na serikali.
Katika kumalizia, Katibu huyo aliomba vijana waendelee kulinda misingi ya amani, ustaarabu na maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa UVCCM itaendelea kuwa jumuiya imara katila kulinda maslahi ya vijana na mustakabali wa Tanzania.
“MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA,†alihitimisha.
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo