UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

CCM YAANZA HARAMBEE YA UCHAGUZI: WANANCHI WAIPOKEA KWA MIKONO MIWILI

12 Aug, 2025 37 Machapisho

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumezindua rasmi harambee ya kuchangia kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kufanikisha kukusanya Shilingi Bilioni 86.31 katika uzinduzi uliofanyika Agosti 12, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Uzinduzi huu umepokelewa kwa shangwe na wananchi, wafanyabiashara, wadau wa maendeleo na wanachama wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan. Katika harambee hiyo, Rais Samia alichangia Sh. Milioni 100, huku Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akichangia Sh. Milioni 50.

Jumla ya fedha taslimu zilizokusanywa ni Sh. Bilioni 56.31, huku Sh. Bilioni 30.2 zikiwa ahadi. Hii ni sehemu ya lengo kubwa la chama kukusanya Sh. Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi wa 2025.

Akizungumza baada ya kupokelewa kwa michango hiyo, Rais Samia alisema:

“Kutoa ni moyo siyo utajiri. Michango yenu ndiyo ngao ya ushindi wetu na dhamira ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.”

Aidha, aliwahimiza wananchi wote kuendelea kushiriki harambee hii, wakiwemo Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).

👉 Jinsi ya Kuchangia kupitia Simu:

  1. Piga: *150*50*1#

  2. Ingiza Control Number: C02025

  3. Weka Kiasi cha Mchango

  4. Ingiza PIN yako kuthibitisha

Michango hii itaendelea kupokelewa hadi Agosti 27, 2025. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewahimiza Watanzania wote wenye mapenzi mema kuendelea kushiriki, akisisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kuandaa ushindi wa chama kinachobeba matumaini ya wananchi