Rais Samia Afanya Mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi
06 Jan, 2026
41 Machapisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 06 Januari, 2026. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi, usalama wa taifa pamoja na mchango wa Jeshi la Kujenga Taifa katika maendeleo ya nchi.
Baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya shughuli rasmi za kiserikali zilizoendelea Ikulu ndogo ya Tunguu.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipata wasaa wa kupiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele. Tukio hilo lilifanyika mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko