Shina la Makunduchi Ladhihirisha kwa Vitendo Kuwa Maendeleo Hayana Itikadi – Dkt. Migiro
20 Jan, 2026
28 Machapisho
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha Rose Migiro, amezindua Shina la Wakereketwa wa CCM Makunduchi lililopo Mtaa wa Uhuru, Wilaya ya Dodoma Mjini, na kulipongeza shina hilo kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza shughuli za kiuchumi zinazolenga kuinua kipato cha wanajamii bila kujali misimamo ya kisiasa.
Akizungumza na wajumbe wa shina hilo Januari 20, 2026, kabla ya kukutana na Mabalozi wa Mashina wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Migiro alisema kuwa hatua iliyochukuliwa na shina hilo inaonesha mshikamano, umoja na uthibitisho wa vitendo kwamba maendeleo ya kiuchumi hayafungwi na itikadi za kisiasa.
“Shina hili niwapongeze sana Mmetuthibitishia kuwa shughuli za kiuchumi hazina itikadi. Kupitia ushirikiano huu, mnawavuta na kuwaunganisha Watanzania na wanajamii wenzetu bila kujali itikadi zao, kwa sababu maendeleo ya nchi hayana itikadi, umoja wa nchi hauna itikadi na uimara wa Taifa letu pia hauna itikadi,” amesema Dkt. Migiro.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa Chama na viongozi wake kushirikiana na jamii nzima, ikizingatiwa kuwa wananchi waliokipigia kura Chama Cha Mapinduzi wanatoka katika makundi tofauti ya kijamii na kisiasa.
“Kura tulizopigiwa zimepigwa na wana CCM na wasiokuwa wana CCM. Rais wetu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama ni Rais wa Watanzania wote, hivyo nasi lazima tuwe watumishi wa wananchi wote,” ameongeza.
Katika hotuba yake, Dkt. Migiro amewataka wanachama wa Shina la Makunduchi kuendelea kuwa kielelezo cha jamii kwa kupiga hatua za mbele kimaendeleo, mshikamano na uzalendo, sambamba na kuchangia katika ujenzi wa Taifa lenye umoja na maendeleo endelevu.
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko