UVCCM KONDODA YAADHIMISHA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA LA VIJANA
31 Jan, 2026
10 Machapisho
KONDOA, TANZANIA – 31 Januari 2026
Leo, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kondoa, Mwalimu Said Ndwata (Bei Chee), ameongoza Kikao cha Kawaida cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya, kilichokuwa na ajenda tatu muhimu kwa maendeleo ya vijana na Jumuiya ya UVCCM wilayani hapa.
Kikao hicho kilifunguliwa na Mhe. Salum Mabote, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kwa niaba ya Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MNEC), Mbunge wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Maliasili na Utalii. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Mabote aliwapongeza vijana kwa ushiriki wao mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, hatua iliyosaidia Chama cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo. Aidha, aliahidi kusaidia Jumuiya ya Vijana kwa kulima shamba lililopo Serya ili kuwawezesha kiuchumi.
Kikao kilifungwa na Ndugu Hassan Dinya, kada wa CCM na mdau wa maendeleo wa taifa. Katika hotuba yake, aliwakumbusha vijana umuhimu wa kuwa mstari wa mbele katika kutimiza malengo na shabaha za CCM, pamoja na kuwekeza nguvu katika kutafuta fursa za maendeleo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Aidha, Ndugu Dinya alitoa mashine ya kupasua, kuranda na kusafisha mbao yenye thamani ya Tsh. 7,000,000/=, lengo likiwa ni kuwawezesha vijana kiuchumi. Mashine hiyo itatumika chini ya vikundi vinavyoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM, huku Ndugu Dinya akiahidi pia kushiriki ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya wakati wa zoezi la uchimbaji wa msingi.
Katibu wa CCM Wilaya, Ndugu Abdulrahim Hamid, aliwashukuru wageni wote kwa kushiriki Baraza na kuwa mstari wa mbele kusaidia Jumuiya. Pia alisisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa sehemu ya kutimiza maazimio yaliyopendekezwa na wagombea wake, huku akiwakumbusha viongozi kulinda mali za Chama na Jumuiya badala ya kuiharibu.
Maadhimisho haya yanathibitisha dhamira ya UVCCM Wilaya ya Kondoa katika kuimarisha mshikamano wa vijana, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kudumisha mshikamano wa Chama Cha Mapinduzi.
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo