UVCCM WILAYA YA KAKONKO WAFANYA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA KUZALIWA KWA CCM
01 Feb, 2026
40 Machapisho
🗒️ Tarehe: 30/01/2026
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kakonko umefanya maadhimisho ya kipekee kuelekea miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM, yatakayofanyika rasmi tarehe 5 Februari 2026. Maadhimisho haya yamejumuisha shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuunga mkono maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Miongoni mwa shughuli zilizofanywa ni:
- Usafi na huduma kwa wagonjwa: Vijana wa UVCCM walishiriki katika usafi wa maeneo ya Zahanati ya Kasuga na kutembelea wagonjwa walioko Zahanati hiyo.
- Kuheshimu wazee: Kutembelea wazee na kutoa zawadi mbalimbali katika vitongoji vya Kewe, Mjini A, Kaganyi, na Kiomoka, wakionyesha heshima na upendo kwa wazee.
- Kupanda miti: Shule ya Msingi na Zahanati ya Kasuga zilipandwa miti kwa lengo la kudumisha mazingira na kukuza elimu ya utunzaji wa mazingira.
Maadhimisho haya yanatolewa kwa kauli mbiu:
"Tumechagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa letu."
#kakonkoYetuKeshoYetu
#TembeaNaCCMKwaKaziYaSamia
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo