UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MOROGORO KUMENOGA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI

04 Feb, 2026 59 Machapisho
Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wameendelea kuonesha mapenzi ya dhati na mshikamano mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea maadhimisho ya miaka 49 tangu kuasisiwa kwake, yanayotarajiwa kufanyika rasmi kesho tarehe 05 Februari, 2026.
Maadhimisho hayo yameanza leo kwa kishindo kikubwa, ambapo mamia ya wananchi, wanachama na vijana wa CCM wamejitokeza kwa wingi kushiriki matembezi maalum ya kuadhimisha miaka 49 ya chama hicho, yakionesha uimara, umoja na mshikamano wa wana-CCM pamoja na wananchi wa Morogoro kwa ujumla.
Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Morogoro, Ndugu Mohammed Ali Kawaida. Uwepo wake umeongeza hamasa na ari kwa wananchi na vijana waliokusanyika kushiriki tukio hilo la kihistoria.
Wananchi waliojitokeza wameeleza kufurahishwa na mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka 49, wakisisitiza kuwa CCM kimeendelea kuwa nguzo ya umoja, amani na maendeleo ya Taifa tangu kuasisiwa kwake hadi sasa. Kauli mbiu za mshikamano, uzalendo na maendeleo zimeendelea kusikika katika matembezi hayo, zikionesha imani kubwa ya wananchi kwa chama chao.
Maadhimisho haya yanaendelea kubeba ujumbe mzito wa “Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa”, yakithibitisha kuwa Morogoro ni sehemu muhimu ya safari ya CCM katika kujenga Tanzania imara, yenye mshikamano na maendeleo endelevu.
Morogoro na CCM ni kitu kimoja, leo, kesho na milele.
 Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.