UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA CCM KIMKOA, WILAYA YA PANGANI

04 Feb, 2026 63 Machapisho
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Halidi Mwinyi, leo anatarajiwa kuongoza sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 49 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya mkoa, zitakazofanyika Wilaya ya Pangani.
Katibu Mkuu UVCCM, Ndugu Halidi Mwinyi alipokea Bendera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Vijana wa CCM Wilaya ya Pangani, waliotekeleza matembezi ya siku saba mfululizo, wakipita katika kata zote 14 za wilaya hiyo, ikiwa ni ishara ya mshikamano, uzalendo na uhai wa chama kuanzia ngazi ya tawi(shina).
Sambamba na hilo, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa alifungua Mashina ya Wakeleketwa wa Umoja wa Vijana wa CCM katika Kata ya Pangani Mashariki, hatua inayolenga kuimarisha misingi ya chama na kuongeza nguvu ya uhamasishaji kwa vijana na wanachama kwa ujumla.
Aidha, alisisitiza kuwa chama ni wanachama na mtaji mkubwa wa chama ni wanachama, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa alishiriki pia katika zoezi la upandishaji wa Bendera ya CCM kwa Mabalozi wa Mashina katika Kata ya Pangani Mashariki, kama ishara ya kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Shina.
Maadhimisho hayo yalifanyika katika hali ya amani, mshikamano na umoja, yakibeba ujumbe wa kuendelea kulinda amani na kuimarisha maendeleo ya Taifa kupitia mshikamano wa Watanzania.
Maadhimisho ya miaka 49 ya CCM yanaongozwa na kauli mbiu isemayo:-
“TUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.”