Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU MKUU UVCCM, HALID MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA CHUO CHA VIJANA IHEMI – IRINGA | UVCCM
Habari Nyingine

KATIBU MKUU UVCCM, HALID MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA CHUO CHA VIJANA IHEMI – IRINGA

04 Mar, 2026 Admin User 39 views min read
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Halid Mwinyi, ametembelea na kukagua maendeleo ya Chuo cha UVCCM Ihemi kilichopo mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Ndugu Mwinyi aliwaeleza viongozi wa UVCCM Mkoa wa Iringa pamoja na Mbunge wa Vijana mkoa huo, Mhe. Jasmine Chesco, umuhimu wa Jumuiya kuunganisha siasa na miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na fursa kwa vijana.
Ziara hiyo iliambatana na tathmini ya hatua zilizofikiwa katika maendeleo ya chuo na uwezekano wa kuboresha miradi ya vijana, ikizingatia mafunzo, uongozi na uzalendo.
#KazinaUtuTunasongaMbele