Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Ndugu ajuaye Msigala Aendeleza ziara ya kitendaji matawini kwa kishindo | UVCCM
Habari Nyingine

Ndugu ajuaye Msigala Aendeleza ziara ya kitendaji matawini kwa kishindo

21 Mar, 2026 Admin User 208 views min read
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Ndugu Ajuaye Msigala, anaendelea na ziara ya kitendaji katika matawi mbalimbali kwa kasi na ari mpya, akilenga kuimarisha uhai wa Jumuiya pamoja na Chama kwa ujumla.
Kupitia ziara hiyo, Msigala amekuwa akishiriki katika matukio mbalimbali na kukutana na vijana katika ngazi za chini, ambapo anapata fursa ya kusikiliza kwa karibu changamoto, maoni na mapendekezo yao. Hatua hii inalenga kuhuisha shughuli za UVCCM na kuongeza ushiriki wa vijana katika utekelezaji wa majukumu ya kijamii na kisiasa.
Ziara hiyo imeambatana na mwitikio mzuri wa vijana, hali inayoonesha kuimarika kwa mshikamano na ari ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza agenda za maendeleo.
#MuhezaKaziInaendelea
#VijanaTupoPamoja