Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU UVCCM (W) SONGEA MJINI AENDELEA NA ZIARA YA KITENDAJI KATA ZA SHULE YA TANGA NA MSHANGANO | UVCCM
Habari Nyingine

KATIBU UVCCM (W) SONGEA MJINI AENDELEA NA ZIARA YA KITENDAJI KATA ZA SHULE YA TANGA NA MSHANGANO

25 Mar, 2026 Admin User 22 views min read
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Songea Mjini, Ndugu David J. Mlonga, ameendelea na ziara ya kitendaji katika Kata za Shule ya Tanga na Mshangano, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli zake.
Katika ziara hiyo, Katibu Mlonga alikutana na vijana pamoja na viongozi wa Jumuiya, ambapo alikagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kuhamasisha mshikamano ndani ya UVCCM. Aidha, aliwahimiza vijana kuitumikia Jumuiya kwa nguvu zote, kwa uzalendo na kujituma, huku akisisitiza umuhimu wa ubunifu wa miradi ya kiuchumi katika ngazi za kata na matawi.
Amesema kuwa kuanzishwa kwa miradi ya kiuchumi kutaiwezesha Jumuiya kuwa na nguvu ya kifedha, hivyo kurahisisha utekelezaji wa shughuli zake bila vikwazo, sambamba na kutoa fursa za maendeleo kwa vijana na jamii kwa ujumla.