Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU UVCCM SONGEA VIJIJINI AFANYA ZIARA YA KIUTENDAJI KUIMARISHA UMOJA WA VIJANA | UVCCM
Habari Nyingine

KATIBU UVCCM SONGEA VIJIJINI AFANYA ZIARA YA KIUTENDAJI KUIMARISHA UMOJA WA VIJANA

25 Mar, 2026 Admin User 48 views min read
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Songea Vijijini ameanza ziara ya kiutendaji katika kata na matawi mbalimbali, akilenga kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuongeza ufanisi wa shughuli za vijana ndani ya chama.
Katika ziara hiyo, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha misingi ya UVCCM kuanzia ngazi ya matawi hadi kata, akibainisha kuwa uimara wa chama unategemea vijana walioandaliwa vizuri na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za kisiasa na maendeleo.
Aidha, amehimiza viongozi na wanachama kuendeleza uandikishaji wa wanachama wapya kupitia mfumo wa kielektroniki ili kurahisisha usajili na kuongeza ushiriki wa vijana ndani ya Jumuiya. Pia amekagua utekelezaji wa vikao vya kikanuni, akisisitiza kufanyika kwake kwa wakati na kwa kuzingatia taratibu ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi.
Sambamba na hilo, Katibu huyo amesikiliza kero na changamoto za vijana katika maeneo mbalimbali na kuahidi kuzifikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Vilevile, amekagua miradi ya vijana na kutoa pongezi kwa matawi yenye jitihada nzuri, huku akihimiza kuongeza bidii ili kufikia malengo ya maendeleo ya Jumuiya na taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo inaendelea katika maeneo mengine ya Wilaya ya Songea Vijijini, ikiwa na lengo la kuhakikisha kila tawi linakuwa hai na linashiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na maendeleo.