Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
UVCCM BABATI VIJIJINI YAENDELEA NA ZIARA KATA ZA QASH NA GALAPO | UVCCM
Habari Nyingine

UVCCM BABATI VIJIJINI YAENDELEA NA ZIARA KATA ZA QASH NA GALAPO

25 Mar, 2026 Admin User 9 views min read
Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Babati Vijijini, chini ya Katibu wa Vijana Ndugu George Sanka, imeendelea na ziara ya kiutendaji katika kata za Qash na Galapo leo tarehe 24/03/2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuongeza ushiriki wa vijana.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha Jumuiya ya UVCCM, kuhamasisha vijana kulipa ada za uanachama, pamoja na kuwajengea uelewa kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi. Miongoni mwa fursa zilizosisitizwa ni pamoja na mikopo inayotolewa kupitia Ofisi ya Rais – Vijana, Wanawake na Wajasiriamali, inayolenga kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.
Katika ziara hiyo, viongozi wamewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za Jumuiya na kuchangamkia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla.
Kulinda na Kujenga Ujamaa
Kazi na Utu Tunasonga Mbele