Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
UVCCM WILAYA YA CHAMWINO YAENDELEA NA ZIARA KATA YA CHILONWA | UVCCM
Habari Nyingine

UVCCM WILAYA YA CHAMWINO YAENDELEA NA ZIARA KATA YA CHILONWA

25 Mar, 2026 Admin User 12 views min read
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Chamwino umeendelea na ziara ya kiutendaji katika Kata ya Chilonwa leo tarehe 24/03/2026, ambapo Katibu wa Vijana amekutana na vijana wa eneo hilo kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kuimarisha shughuli za Jumuiya.
Katika ziara hiyo, Katibu alipata fursa ya kukusanya kero mbalimbali zinazowakabili vijana pamoja na kukagua maeneo yatakayotumika kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali (kambi) kwa vijana, hatua inayolenga kuwawezesha kiujuzi na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za maendeleo.
Ziara hiyo inaendelea kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha uhai wa Jumuiya na kujenga msingi imara wa vijana wenye uwezo na ari ya kulijenga taifa.
Kazi na Utu Tunasonga Mbele
Taifa Letu, Amani Yetu