Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
ZIARA YA KITENDAJI KATIBU UVCCM (W) KIBAHA MJINI – VIJANA TUONGEE FURSA | UVCCM
Habari Nyingine

ZIARA YA KITENDAJI KATIBU UVCCM (W) KIBAHA MJINI – VIJANA TUONGEE FURSA

26 Mar, 2026 Admin User 34 views min read
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ndugu Joel Jacob Kituu, ameanza rasmi ziara ya kitendaji inayojulikana kwa jina la “Vijana Tuongee Fursa” katika Kata ya Tangini.
Ziara hiyo inalenga kuthibitisha uhai wa Jumuiya, kusimamia usajili wa wanachama kwa mfumo wa kielektroniki, na kutoa elimu kwa vijana kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika Manispaa ya Kibaha.
Aidha, Katibu Kituu amewahamasisha vijana kushirikiana na Afisa Viwanda na Biashara pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa katika kujifunza na kuchangamkia fursa hizo, ili kuongeza ufanisi wa kijamii na kiuchumi kwa vijana