Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
UVCCM KAGERA YAMPOKEA KATIBU WA SIASA, ITIKADI NA UENEZI TAIFA KWA SHANGWE | UVCCM
Habari za Wilaya

UVCCM KAGERA YAMPOKEA KATIBU WA SIASA, ITIKADI NA UENEZI TAIFA KWA SHANGWE

27 Mar, 2026 Admin User 35 views min read
Bukoba, Kagera
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Kagera umempokea kwa heshima na shangwe Ndugu Kenani Kihongosi, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi Taifa, katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Ujio wa kiongozi huyo umeelezwa kuwa ni kielelezo cha dhamira thabiti ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha itikadi, mshikamano na maendeleo ya vijana nchini.
Akizungumza katika mapokezi hayo, viongozi wa UVCCM Mkoa wa Kagera chini ya Mwenyekiti Ndugu Faris Buruhani wamebainisha kuwa ujio huo unaimarisha ari na mwelekeo wa vijana katika kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na ujenzi wa taifa.
Ziara hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi na vijana, sambamba na kukuza uelewa wa itikadi ya chama na fursa mbalimbali za maendeleo kwa vijana wa Mkoa wa Kagera.