Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI BARAZA KUU UVCCM, ENG. DEBORA TLUWAY AFUNGUA UNI-SUMMIT MKOA WA MBEYA | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM)

MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI BARAZA KUU UVCCM, ENG. DEBORA TLUWAY AFUNGUA UNI-SUMMIT MKOA WA MBEYA

13 Jun, 2026 Admin User 21 views min read

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Ndugu Eng. Debora Joseph Tluway, leo amefungua rasmi Uni-Summit Mkoa wa Mbeya, jukwaa linalowakutanisha wanafunzi wa elimu ya juu kwa lengo la kujengeana uwezo, kubadilishana uzoefu na kuhamasishana kutumia elimu katika kuleta maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Eng. Debora aliwahimiza wanafunzi kuitumia Uni-Summit kama fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali, kujenga mitandao ya kitaaluma (professional networking), kuchangamkia fursa za maendeleo na kuendelea kukuza stadi zitakazowawezesha kuwa na ushindani katika soko la ajira na ujasiriamali.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa uzalendo kwa vijana, akieleza kuwa elimu inapaswa kuwa nyenzo ya kuibua fikra bunifu, kutoa suluhisho kwa changamoto za jamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

Eng. Debora pia aliwataka vijana kutumia maarifa wanayoyapata vyuoni kuleta mabadiliko chanya katika jamii zinazowazunguka, huku wakishiriki kikamilifu katika kulinda amani, umoja na utulivu wa Tanzania, ambavyo ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu.

Uni-Summit Mkoa wa Mbeya imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwawezesha vijana kukuza uwezo wao wa kitaaluma, ubunifu na uongozi, sambamba na kuwajengea mtandao utakaowawezesha kunufaika na fursa mbalimbali za maendeleo.