Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
WASOMI WA MKOA WA MWANZA WAMUHAIDI KATIBU MKUU UVCCM MWINYI, HAWATA SHAWISHIKA KUHARIBU AMANI YA NCHI | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

WASOMI WA MKOA WA MWANZA WAMUHAIDI KATIBU MKUU UVCCM MWINYI, HAWATA SHAWISHIKA KUHARIBU AMANI YA NCHI

21 Jun, 2026 Admin User 17 views min read

Wasomi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu vya Mkoa wa Mwanza wamemuahidi Katibu Mkuu wa UVCCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Halid Mwinyi kwamba watakuwa mabalozi wa amani katika Mkoa wa Mwanza na Taifa kijumla, wakijikita katika kuelimisha jamii kuhusu thamani ya amani na mchango wake katika maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla.

Wasomi hao wametoa ujumbe huo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Mwanza, ambapo katibu Mkuu UVCCM Halid Mwinyi(MNEC) alishiriki kama Mgeni Rasmi. Wamesisitiza kuwa hawatashawishika kushiriki au kuunga mkono mienendo yoyote inayoweza kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa, bali wataendelea kuwa sehemu ya suluhisho kupitia elimu, uelewa na ushirikiano wa kijamii.


Tukio hilo limefanyika leo Jumapili, tarehe 21 Juni 2026, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Mwanza.

#KaziNaUtuTunasongaMbele

#NeverAgain