Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU MKUU UVCCM MWINYI AWAALIKA WASOMI KUKAA MKAO WA KULA NYONGEZA YA BAJETI YA TSH TRILIONI 1.07 YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2026/27 | UVCCM
Habari za Kitaifa (UVCCM) Kipaumbele

KATIBU MKUU UVCCM MWINYI AWAALIKA WASOMI KUKAA MKAO WA KULA NYONGEZA YA BAJETI YA TSH TRILIONI 1.07 YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2026/27

21 Jun, 2026 Admin User 25 views min read

Mwanza, Juni 21, 2026

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Ndugu Halid Mwinyi, amewaalika wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu pamoja na wale wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2026/27 kukaa mkao wa kula kufuatia ongezeko kubwa la Bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu lililopendekezwa na Serikali.

Akizungumza leo, Juni 21, 2026, akiwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), jijini Mwanza, Ndugu Mwinyi alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwekeza katika elimu na maendeleo ya vijana.

Amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, ambapo fedha za Mikopo ya Elimu ya Juu zinatarajiwa kuongezeka kutoka Shilingi Bilioni 917 mwaka 2025/26 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.07 mwaka 2026/27.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, bajeti hiyo inatarajiwa kuwanufaisha takribani wanafunzi 280,000, ikilinganishwa na wanafunzi 252,773 walionufaika mwaka 2025/26. Hii ni nyongeza ya zaidi ya Shilingi Bilioni 153, sawa na ongezeko la asilimia 16.7.

Ndugu Mwinyi amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata fursa ya elimu ya juu kupitia mfumo wa mikopo.

Aidha, amewataka wanafunzi na wazazi kuendelea kuwa na imani na Serikali ya CCM huku wakiendelea kudumisha amani ya Taifa letu

#KaziNaUtuTunasongaMbele

#NeverAgain

#FyuchaBilaStresi