UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

UVCCM HAKUNA KUPOA, TUTAFIKA KILA KONA NA WAGOMBEA WETU

04 Sep, 2025 63 Machapisho
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Ndg. Mussa Mwakitinya akiwa ameambatana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Ivan Moshi na Mkuu wa Idara ya Uhusiano Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu, Ndg. Emanuel Martine wameendelea kumuunga mkono Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiendelea na kampeni mkoani Shinyanga.

 Leo tarehe 04 Septemba 2025 Balozi Dk. Nchimbi yupo wilaya ya Kahama eneo la Kagongwa, Isaka na Ushetu ambapo viongozi hao wa UVCCM wanaobeba dhamana ya Vijana wamehakikisha vijana wanajaa kwa wingi kusikiliza sera za CCM ambazo zinagusa maendeleo yao ikiwemo ajira, afya, elimu na miundombinu.

#oktonatunatiki
#kazinaututunasongambele
#tunazimazotetunawashakijani
#fyuchabilastresi