UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT. SAMIA KIONGOZI MWENYE UPENDO

04 Sep, 2025 39 Machapisho
 Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye upendo kwa wananchi wake, anayejali utu na maisha bora ya kila Mtanzania. Upendo huu umejidhihirisha kupitia maamuzi yake ya kuwekeza zaidi kwenye afya, elimu, maji safi, nishati, miundombinu na uwezeshaji wa vijana na wanawake na maendeleo kiujumla.

Chini ya Ilani ya CCM 2020–2025, Tanzania tumeshuhudia mageuzi makubwa ya maendeleo yanayogusa maisha ya watu wote. Dkt. Samia ni Mama wa Maendeleo na mlezi wa taifa, anayesimamia sera zenye kugusa maisha ya kila mmoja kwa usawa.

Wananchi wanaojitokeza kwa maelfu kila anapopita ni ushahidi kwamba upendo wake umewagusa, na imani yao kwake ni ya kweli.
“Oktoba 29 tunamtiki Dkt. Samia – Kiongozi mwenye upendo, Mama wa Maendeleo.”

#KiongoziMwenyeUpendo
#DktSamiaMamaWaMaendeleo