KISHINDO CHA DKT.NCHIMBI NYANG'HWALE NI USHINDI TU
05 Sep, 2025
68 Machapisho
Maelfu ya wananchi wa Nyang’hwale, mkoani Geita leo Septemba 5, 2025 wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Saba Saba kumpokea na kumsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiendelea na mikutano ya kampeni za CCM. Mapokezi hayo yameonesha imani kubwa ya wananchi kwa CCM na kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa CCM.
Akihutubia wananchi, Dkt. Nchimbi amewataka kujiandaa kwa Oktoba 29 kuhakikisha kura zote za kishindo ni za CCM. Amebainisha kuwa chama hicho kimeendelea kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli kupitia miradi ya afya, elimu, kilimo, viwanda na nishati, hivyo wananchi hawana sababu ya kuyumba. Pia aliwanadi wagombea wa ubunge na udiwani akiwemo Hallen Nassor Amar (Buldoza), Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nyang’hwale.
Wananchi wa Nyang’hwale walilipuka kwa shangwe na hamasa kubwa wakiahidi kwa sauti moja kuwa hawatapoteza kura hata moja nje ya CCM. Nyang’hwale waapa kuwa 29 Oktoba ni ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia na ubunge CCM na kwa madiwani wa CCM.
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazimaZoteTunawashaKijani
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.