UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

WANAVYUO CHAGUA CCM, CHAGUA SAMIA,SAMIA ASHINDE KWA KISHINDO

22 Sep, 2025 14 Machapisho
Mkuu wa idara ya uhusiano ya Kimataifa vyuo na vyuo Vikuu UVCCM Taifa *Ndg Emanuel Martine* Leo tarehe 22/09/2025 amekutana na kuzungumza na Timu ya ushindi ya vijana wanavyuo wa vyuo vya kati na vyuo vikuu, viongozi mbalimbali na walezi wa matawi ya vyuo na vyuo vikuu katika mkoa wa Dar es salaam wanaoendelea kuzisaka kura za *Dkt Samia Suluhu Hassan* mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mgombea mwenza wake *Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi,* wabunge na Madiwani wa CCM.


Ndg Emanuel Martine amewasisitiza wanavyuo kuzitafuta kura za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan mtu kwa mtu, simu kwa simu, mitaa kwa mitaa, nyumba kwa nyumba, vijiwe kwa Vijiwe na makundi kwa makundi ili kuhakikisha Kura za Dkt Samia Suluhu Hassan zinapatikana kwa wingi, Samia ashinde kwa kushindo *(fact and figure)*

Chama Cha Mapinduzi na wanavyuo ni chanda na pete, wanavyuo wanakipenda Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Mapinduzi kinawapenda wanavyuo kutoka vyuo vya kati na vyuo Vikuu 

#WanavyuoChaguaCCMChaguaSAMIA
#FurahayetuSamiawetu2025-2030
#KaziNaUtuTunasongaMbele