UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MWINYI AKUTANA NA FIRST TIME VOTERS NANGWA

22 Sep, 2025 16 Machapisho
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa Ndugu Halid Mwinyi amekutana na kuzungumza na Vijana ambao wanatarajia kupiga kura kwa mara ya kwanza (First Time Voters) wa Chuo cha Ufundi cha Nangwa leo tarehe 22 Septemba, 2025 Wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.

Katika mazungumzo yake, Ndugu Mwinyi amewasihi kuzingatia mafunzo wanayoyapata chuoni hapo kwani ndio msingi pekee utakaowawezesha kukabiliana vyema na uchangamoto za ajira na kujikwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo, aliwasisitiza kutambua haki zao za msingi kwani ndio mara yao ya kwanza kushiriki uchaguzi Mkuu hivyo wana wajibu wa kuchagua Viongozi sahihi ambao wanaamini watawawezesha kufikia malengo yao katika jamii inayowazunguka.

Vijana tunasema,
Oktoba ni mwendo wa kutiki ✅ kwa sababu CCM imetuhakikishia fyucha bila stresi.

#OktobaTunatiki✅✅
#FyuchaBilaStresi
#KaziNaUtuTunasongaMbele