UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

NYONGEZA YA MSHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA, CHACHU YA UPENDO WA WATUMISHI KWA DKT. SAMIA

28 Sep, 2025 28 Machapisho

Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa, Ndg. Emanuel Martine, leo tarehe 28/09/2025 amekutana na walimu makada na wazalendo wa Mkoa wa Iringa akiwa ameambatana na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Ndg. Bulugu Magege.

Katika mkutano huo, Ndg. Emanuel Martine amewataka walimu na watumishi wa umma kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumpa kura  kwa kishindo sambamba na kuwapigia kura wabunge na madiwani wote wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Waalimu makada wazalendo wa Iringa wametoa ahadi ya dhati ya kumpa kura nyingi za kishindo mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakieleza wazi kuwa nyongeza za mshahara na maboresho aliyoyafanya yamegusa moja kwa moja maisha yao na kuboresha ustawi wa watumishi wote wa umma nchini.

Kabla ya kikao hicho, Ndg. Emanuel Martine alishiriki pia katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Iringa, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ndg. Agrey Tonga. Kikao hicho kilijadili kwa kina mikakati ya kuhakikisha ushindi wa kishindo wa CCM na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa mzima wa Iringa kupitia nguvu ya vijana.

Hakika, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mama mnyenyekevu, mchapa kazi, mwenye upendo wa kweli kwa wananchi wake. Sasa ni wakati wa kila Mtanzania, hususan vijana na walimu, kuhakikisha anapewa kura nyingi tarehe 29/09/2025 ili kuendeleza kazi kubwa na njema alizoanzisha.

#OktobaTunatiki✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazazoteTunawashaKijani
#WanavyuoChaguaCCMChaguaSAMIA