VIJANA SHINYANGA WAFUNIKA, WAMUAPISHA DKT. SAMIA KWA KISHINDO CHA OKTOBA TUNATIKI
11 Oct, 2025
44 Machapisho
ðŸ—“ï¸ Tarehe 11/10/2025
ðŸ“kahama-Shinyanga
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC), ameongoza maelfu ya vijana wa Shinyanga Mjini katika matembezi ya kishindo yaliyojaa hamasa, uzalendo na mshikamano chini ya kaulimbiu ya Oktoba Tunatiki Vijana hao wameonesha umoja wa nguvu ya kizazi kipya, wakiahidi kulinda amani, kudumisha utulivu wa Taifa na kujitoa kwa dhati kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 29 Oktoba 2025, wakisema ndiye kiongozi anayewaletea matumaini, Maendeleo,na Tanzania yenye usawa kwa wote.
Katika tukio hilo lililogeuka kuwa sherehe ya umoja na matumaini ya vijana, sauti za “Tunatiki!†zilitawala mitaa yote ya Shinyanga, zikibeba ujumbe wa imani kwa uongozi wa Dkt. Samia na ahadi ya kuendeleza juhudi zake za kujenga Tanzania yenye fursa, ajira na ustawi wa vijana Shinyanga imetoa Taswira ya Taifa lililo tayari kwa uchaguzi wa amani, huku vijana wakiahidi kuendelea kuwa nguzo imara ya ushindi wa CCM na uendelevu wa maendeleo chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
#OktobaTunatiki✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNiTokeTukaTiki✅
Habari Zinazohusiana
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR
09 Feb, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
RAIS DKT. SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA ELIMU YA ZIMAMOTO SOKO JIPYA LA KARIAKOO
08 Feb, 2026
Dar es Salaam 08 Februari 2026 Katika kulinda uwekezaji wa umma na kuhakikisha thamani ya fedha za wananchi inalindwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kutunza na kusimamia miundombinu ya Soko
RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SOKO JIPYA LA KARIAKOO: AFUNGUA UKURASA MPYA WA TUMAINI LA KIUCHUMI, AAGIZA HAKI, UWAZI NA USALAMA KWA WAFANYABIASHARA
08 Feb, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Jengo Jipya la Soko la Kariakoo