UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

UVCCM YASHIRIKI WIKI YA VIJANA KITAIFA MKOANI MBEYA

11 Oct, 2025 15 Machapisho

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeshiriki katika wiki ya Vijana inayoendelea Jijini Mbeya, ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 10 Oktoba 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).

Banda la UVCCM linatoa huduma  mbalimbali zenye lengo la kuwaelimisha vijana wa Kitanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki uchaguzi na kutumia haki yao ya kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025, ikiwemo elimu ya namna sahihi ya kumchagua Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kura ya kishindo 

Huduma nyingine zinazotolewa ni pamoja na elimu juu ya Mfumo wa Kijani IlaniChatbot (Ilani ya CCM Kidijitali kwa Vijana), usajili wa kielektroniki wa wanachama wa CCM, huduma ya kurejesha namba za kielektroniki kwa waliopoteza, pamoja na kutoa elimu ya uzalendo na umuhimu wa amani ya Taifa letu. Vijana wamejitokeza kwa wingi kutembelea banda la UVCCM, wakipata huduma na elimu ya kisiasa kwa vitendo.

#KazinaUtuTunasongaMbele ✅
#TokaNitokeTukatiki ✅
#OktobaTunatiki ✅
#TunazimazoteTunawashaKijani ✅