UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MATEMBEZI YA HESHIMA KUELEKEA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI BUKOMBE

12 Oct, 2025 11 Machapisho
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) ameongoza matembezi ya maelfu ya vijana wa Bukombe mkoani Geita kuelekea Uwanjani ambapo unafanyika mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Oktoba 2025.

Ndg. Kawaida ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Ndg. Mussa Mwakitinya, Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Ndg. Jessica Mshama, Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita, Ndg. Manjale Magambo na Mgombea wa Ubunge Arusha Mjini, Ndg. Paul Makonda ambapo maelfu hayo ya vijana wamesema kura zao zote ni kwa Dkt. Samia Oktoba 29.

#OktobaTunatiki✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukaTiki✅