UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Nafidh Ally Mola

Nafidh Ally Mola

Umri: 20 Dar es Salaam, Tanzania Computer Science / TEHAMA (Mbunifu na Developer mwenye utaalamu wa vitendo katika teknolojia na AI)
Nafidh Ally Mola ni kijana mbunifu wa teknolojia na akili mnunde (AI) kutoka Tanzania mwenye umri wa miaka 20. Ametambuliwa kitaifa na kimataifa kwa ubunifu wake katika TEHAMA, ikiwa ni pamoja na kushiriki Global Misk Forum na kutunukiwa tuzo ya Best AI Innovator in Africa kupitia AUDA-NEPAD. Ni kijina mbunifu na mwenye mawazo chanya ya kutumia teknolojia katika kutatua changamoto za jamii

Historia na Wasifu

Nafidh Ally Mola ni zao la nidhamu, bidii na maamuzi sahihi aliyoyafanya tangu akiwa shuleni ya Msingi. Alianza safari yake ya teknolojia mapema baada ya kugusa kompyuta kwa mara ya kwanza, jambo lililomfungulia mlango wa kujifunza kwa vitendo. Akitumia muda wake mwingi kufanya majaribio na kujifunza binafsi, alijitokeza kuwa mmoja wa wanafunzi bora katika masomo ya TEHAMA na baadaye kutambuliwa kitaifa katika Computer Science kwa ngazi ya sekondari. Umahiri wake ulimfikisha kutwaa tuzo mbalimbali za ubunifu, ikiwemo Youth Expo Award, kabla ya kushinda tuzo ya kitaifa ya Developer Programmer. Mafanikio yake yalivuka mipaka ya nchi alipoiwakilisha Afrika Mashariki katika Global Misk Forum, na hatimaye kutunukiwa heshima ya Best AI Innovator in Africa kupitia AUDA-NEPAD. Pamoja na mafanikio hayo, Nafidh amejikita kuwainua vijana wenzake kupitia elimu ya TEHAMA, usalama mtandaoni na ujasiriamali wa kidijitali.

Mafanikio

i. Kushiriki na kuzungumza katika Global Misk Forum
ii. Mwnafunzi Bora kitaifa katika Computer Science (ngazi ya sekondari)
iii. Tuzo bora ya Youth Expo Award
iv. Tuzo ya kitaifa ya Developer Programmer
Best AI Innovator in Africa – AUDA-NEPAD
v. Mbunifu bora Mkoa wa Dar es Salaam

Changamoto Nilizopita

i. Kujifunza teknolojia kwa rasilimali chache
ii. Umri mdogo kutokupewa uzito katika hatua za mwanzo
iii. Kujifunza kwa bidii bila kukata tamaa licha ya vikwazo

Ushauri kwa Vijana Wengine

Vijana wasiogope kuanza wakiwa wadogo, waheshimu muda, wajenge nidhamu na waamini kuwa teknolojia inaweza kuwa daraja la mafanikio bila kusubiri kuajiriwa.
Rudi kwa Vijana Wenye Mafanikio