Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Semina ya Makatibu wa Kata UVCCM Kibaha mjini yafanikisha uwezeshaji wa kijana | UVCCM
Habari Nyingine

Semina ya Makatibu wa Kata UVCCM Kibaha mjini yafanikisha uwezeshaji wa kijana

21 Mar, 2026 Admin User 27 views min read
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ndugu Joel J. Kituu, ameongoza semina maalumu kwa Makatibu 14 wa UVCCM Kata za Kibaha Mjini, lengo likiwa kuongeza ujuzi na uwezo wao wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Semina hii, iliyofatiwa na kikao cha kazi, imezaa matokeo chanya kwani imekuja na mpango mpya wa "VijanaTuongeeFursa" utakaotekelezwa kupitia Ziara ya Kitendaji kuanzia tarehe 26 Machi 2026 hadi 2 Aprili 2026. Mpango huu unalenga kuimarisha uhusiano wa vijana na kutoa mwongozo wa kimaslahi na fursa za maendeleo.
Katibu Kituu amesisitiza umuhimu wa "Kulinda na Kujenga Ujamaa" katika kila kitendo cha kijana, akihimiza mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu. majukumu.
#VijanaTuongeeFursa