UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MKUU WA MKOA WA SONGWE AFURAHISHWA NA UBUNIFU WA UVCCM KUPITIA MFUMO WA “KIJANI ILANI CHATBOT

15 Oct, 2025 17 Machapisho
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Jabiri Omari Makame, ametembelea banda la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyotamatika katika Viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025 na kutoa pongezi kwa ubunifu wa kidijitali uliofanywa na vUVCCM chini ya uongozi bora wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC).

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mheshimiwa Makame  ambaye pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa (2012–2015)  amepongeza mfumo wa kisasa wa “Umoja wa Vijana wa Ilani ya CCM  Kijani Ilani Chatbot”, akisema ni njia bora na ya ubunifu wa habari na mawasiliano inayowawezesha vijana kujifunza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020–2025 na kujua malengo ya Ilani ijayo ya CCM 2025–2030 kwa urahisi zaidi kupitia teknolojia.

Ameeleza kuwa Kijani Ilani Chatbot ni mfano wa mwelekeo mpya wa  UVCCM katika kutumia TEHAMA kama nyenzo ya elimu, ushirikishwaji, na mawasiliano.

Makame ameongeza kuwa: “Msingi wa Mwenge wa Uhuru ni Umoja wa Vijana wa CCM, na ndiyo maana nembo ya UVCCM ina Mwenge wa Uhuru.”

KAULI MBIU:
💪 NGUVU KAZI YA VIJANA KWA MAENDELEO ENDELEVU 

SHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025 KWA AMANI NA UTULIVU

#KazinaUtuTunasongaMbele ✅
#TokaNitokeTukatiki ✅
#OktobaTunatiki ✅
#TunazimazoteTunawashaKijani ✅