UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

JESSICA MSHAMA AONGOZA MATEMBEZI YA HAMASA MULEBA

15 Oct, 2025 21 Machapisho
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Ndg. Jessica Mshama, ameongoza matembezi ya maelfu ya vijana wa hamasa wilayani Muleba, mkoani Kagera, leo tarehe 15 Oktoba 2025, kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Vijana hao walishiriki kikamilifu katika matembezi hayo na kwa hamasa ya pamoja, wakionyesha imani yao kubwa kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM  Dkt. Samia Suluhu Hassan na mchango wake katika maendeleo ya Muleba. Ndg. Jessica Mshama aliwataka vijana wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, kuhakikisha wanatiki kwa kishindo kumchagua Mgombea wa Urais, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi za ubunge na madiwani.

Matembezi haya yamethibitisha mshikamano wa vijana, dhamira yao ya kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu, na kujitolea kwa maendeleo endelevu ya taifa.

✅ #OktobaTunaTiki
✅ #FyuChaBilaStresi
✅ #TokaNiTokeTukaTiki