MRADI WA MAJI WA ZIWA VIKTORIA KUWANUFAISHA WANAMULEBA
15 Oct, 2025
17 Machapisho
🗓️ 15 Oktoba, 2025
📍Muleba-Kagera
Ahadi za Dkt. Samia Suluhu Hassan zinaendelea kutafsiriwa kwa vitendo kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, ikiwemo mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Viktoria unaoelekezwa hadi Wilaya ya Muleba.
Mradi huu ni ushahidi wa dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za kijamii bila Ubaguzi wa kijiografia, kijinsia au kipato, Kupitia mradi huu, maelfu ya wananchi wa Muleba watanufaika kwa kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta Maji, huku pia Ukichochea afya bora, uchumi wa kaya na maendeleo endelevu kwa jamii nzima Huu ndiyo ushahidi wa uongozi makini unaotekeleza kwa vitendo falsafa ya “Kazi Iendelee, Maisha Yaboreke.”
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.