UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA CHUO CHA VETA KYAKA

15 Oct, 2025 7 Machapisho
🗓️ Tarehe 15 Oktoba,2025
📍Muleba-Kagera

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Mkutano wa kampeni Uliofanyika Muleba, ameeleza dhamira ya Serikali kukamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Kyaka, hatua itakayowezesha vijana wa Kagera kupata mafunzo bora ya ufundi stadi na kujiajiri. 

Amesisitiza kuwa chuo hicho kitakuwa sehemu ya mkakati wa serikali wa kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kisasa, kuongeza ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa Ziwa, sambamba na kuijenga Tanzania yenye msingi wa ujuzi na ubunifu.

#OktobaTunatiki✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki✅