DKT. SAMIA: TUMEMPOTEZA KIONGOZI MAHIRI NA MPENDA AMANI
15 Oct, 2025
6 Machapisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, akimtaja kuwa kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu.
Amesema Raila alikuwa na ushawishi na upendo uliovuka mipaka ya Kenya na kwamba msiba huu sio wa Wakenya pekee, bali pia ni wa Watanzania na Waafrika wote.
“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa Rais wa Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, Mama Ida Odinga, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Kenya kwa msiba huu,” amesema Rais Dkt. Samia.
Aidha, Rais Samia ameungana na familia ya Odinga kuwaombea faraja, subra na imani katika kipindi hiki kigumu, huku akiomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga mahali pema peponi, Aamiin .
#KazinaUtuTunasongaMbele
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki.
#TunazimaZoteTunawashaKijani
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.