UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI KUKAMILISHA TAWI LA CHUO KIKUU CHA UDSM KAGERA

16 Oct, 2025 9 Machapisho
🗓️ Tarehe 16 Oktoba,2025
📍Bukoba Mjini-Kagera

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Ndugu Samia Suluhu Hassan akiwa Bukoba Mjini, Mkoa wa Kagera, amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu ya juu kwa kukamilisha tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kagera hatua itakayokuza fursa za elimu, kuongeza utafiti na kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Ukanda wa ziwa. 

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Serikali kuhakikisha elimu bora inapatikana karibu na wananchi wote bila kujali umbali wala hali zao za kiuchumi, Aidha amesisitiza kuwa Uwepo wa chuo hicho Utachochea ajira, ubunifu na Maendeleo Endelevu katika Mkoa wa Kagera.

#oktobatunatiki✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅