UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

FARIS BURUHANI AHAIMIZA VIJANA WA KAGERA KUSHIRIKI UCHAGUZI NA KUMCHAGUA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

17 Oct, 2025 12 Machapisho
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, ameeleza kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta mafanikio makubwa kwa vijana, ikiwemo kuinua sekta ya kilimo, maendeleo ya elimu, fursa za ajira na uongozi, pamoja na huduma bora za afya.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukoba, Faris aliwahimiza vijana kushiriki uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, kwa amani na utulivu, na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa CCM wa ubunge na madiwani.

Faris alimshukuru Rais Samia kwa namna anavyoendelea kuwathamini na kuwapa nafasi vijana katika uongozi wa kitaifa, akibainisha kuwa uongozi wake umeleta matumaini makubwa kwa kizazi kipya cha Watanzania.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt. Samia, bei ya kahawa, zao kuu la biashara mkoani Kagera  imepanda kwa kiwango kikubwa, hali iliyowawezesha vijana wengi kuinuka kiuchumi kupitia sekta ya kilimo. Rais Dkt.Samia amekuwa akiwajali na kuwathamini Watanzania wote hasa vijana.