UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT SAMIA AWAPONGEZA VIJANA WA HAMASA

17 Oct, 2025 8 Machapisho
🗓 Alhamisi 16 Oktoba 2025 
📍 Bukoba Mjini 

Mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akihitimisha Ziara yake Mkoani Kagera amefanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Bukoba Mjini na kuwashukuru viongozi wa chama, wananchi vijana wa hamasa na makundi yote kwa ujumla kwa mapokezi na ushiriki wao mzuri wa mikutano yake ndani ya mkoa huo.

Aidha kwa upekee ametoa pongezi za dhati kwa makundi ya hamasa kwa kuchangamsha mikutano na kuwafanya watu kufurahia na kusikiliza kwa umakini yote mazuri ya Chama cha mapinduzi, pongezi hizi ni wazi kabisa zinaonesha uimara na maandalizi mazuri ya Jumuiya ya UVCCM Taifa chini ya Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) ambae amekuwa mstari wa mbele wakati wote kwa vijana.

#OktobaTunatiki ✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki✅