UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MRADI WA ZIWA TANGANYIKA KUTATUA KERO YA MAJI RUKWA

18 Oct, 2025 6 Machapisho
🗓️ Jumamosi Tarehe 18 Oktoba,2025
📍Nkasi-Rukwa

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali imeweka mpango kabambe wa kutatua changamoto ya maji mkoani Rukwa kupitia Mradi Mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Tanganyika, mradi utakaonufaisha maelfu ya wananchi wa Sumbawanga, Nkasi na Kalambo. 

Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kutatua kero za Msingi kwa vitendo, Ikiwemo maji safi, afya na miundombinu ili kuhakikisha wananchi wa Rukwa Wanaishi kwa heshima na Maendeleo Endelevu.

#oktobatunatiki✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅