UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

29 OKTOBA TUNATIKI AFYA YA MAMA NA MTOTO

18 Oct, 2025 6 Machapisho
🗓️Jumamosi Tarehe 18 Oktoba,2025
📍Nkasi-Rukwa

Ni wakati wa kizazi kipya cha vijana wa CCM kusimama imara kwa mustakabali wa Taifa lenye afya bora kwa wote, Tukithibitisha kwa vitendo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. 

Kupitia ujenzi wa vituo vya afya, upatikanaji wa dawa, na huduma za uzazi salama, Tanzania inajenga msingi wa kizazi chenye uhai, Matumaini na ustawi, Tunaamini mama mwenye afya ni uti wa mgongo wa familia mtoto mwenye huduma bora ni kesho ya taifa. Kila kura ni uhai, kila tikii ni ahadi ya upendo kwa vizazi vijavyo Samia anatekeleza sisi vijana tunathibitisha.

#oktobatunatiki✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅