UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI YA CCM KUJENGA UZIO WA MAFURIKO RUFIJI

20 Oct, 2025 10 Machapisho
Rufiji-Pwani,Katika mkutano uliojaa hamasa na matumaini mapya kwa wananchi wa Rufiji, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza mpango kabambe wa serikali wa kujenga uzio maalum wa kuzuia mafuriko katika bonde la Rufiji. 

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya CCM kuhakikisha wananchi wanaishi kwa usalama na shughuli za kilimo, biashara na makazi haziathiriwi tena na maafa ya mvua kubwa, Dkt. Samia amesisitiza kuwa serikali itasimamia utekelezaji wake kwa vitendo ili kulinda maisha ya Watanzania na kuendeleza kasi ya maendeleo endelevu nchini.

#oktobatunatiki✅✅✅
#fyuchabilastresi 
#tokanitoketukatiki ✅