UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT SAMIA TUNA KAMPUNI ZAIDI YA NNE (4) ZA USAFIRI MWENDOKASI DAR

22 Oct, 2025 5 Machapisho
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa tiketi ya CCM *Dkt. Samia Suluhu Hassan,* ameonyesha dhamira thabiti ya kuboresha huduma za usafiri jijini Dar es Salaam kupitia mfumo wa Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi (UDART). Hivi karibuni, Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na kampuni nne kuendesha huduma za mabasi katika njia zinazofikia vituo vya mwisho vya mwendokasi

Uwepo wa kampuni hizi unatarajiwa kuongeza ufanisi na ushindani chanya katika sekta ya usafiri wa umma, kupunguza msongamano wa abiria katika vituo, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, za haraka na zenye bei nafuu. Hatua hii pia inafungua fursa za ajira kwa vijana, kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa kuboresha mtiririko wa watu na biashara katika jiji la Dar es Salaam.

#OktobaTunatiki✅✅✅
#TokaNitokeTukatiki✅
#FyuchaBilaStresi